Kampuni ya SG Entertainment inayoandaa mashindano ya Urembo katika Kitongoji cha Chang’ombe Wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam, imefanya utambulisho rasmi leo Mei 30.2016 mbele ya wanahabari juu ya maandalizi ya shindano hilo ambapo fainali yake itafanyika tarehe 21/07/2016 katika viwanja vya CDS Park zamani ikiitwa TCC Club pale Chang’ombe.
Akizungumza kwenye utambulisho huo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Bwana. Victor Mkumbo amebainisha kuwa, warembo watano kutoka Chang’ombe wataungana na warembo kutoka vitongoji vingine viwili Kigamboni na Mbagala kuwatafuta warembo wa Temeke na baadaye Mrembo wa Tanzania kwa mwaka huu wa 2016.
Victor Mkumbo amebainisha kuwa, Miss Chang’ombe 2016 inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 02/06/2016 kuanzia saa 2, usiku Alhamisi katika ukumbi wa MPOAFRIKA uliopo Davis Corner Tandika.
“Katika uzinduzi huo warembo watatambulishwa na kupita mbele ya wageni watakaoudhuria huku wakisindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo GALATONE na mwanadada CHEMIKAL. Uzinduzi huu si wa kukosa kwani utakuwa ni wa aina yake na utapambwa na ‘surprise’ za kutosha kutoka kwa wadau na wadhamini” alieleza Victor Mkumbo.
Aliwataja baadhi ya warembo watakaoshiriki kweye kinyang’anyiro hicho ni paamoja na :
Neema Ogote (20), SitiZuhura Hussein (20), Hadija Salum (18), Anitha Mugisha (19), Dorothea Shayo (20), Anna Mtua (20), Rehema Mongi(21) na Esther Mnuhi(22).
Kwa upande wake, mratibu wa shindano hilo, Bwana Adam Hussein ameeleza kuwa, bado nafasi za warembo kushiriki ziko wazi, amewaomba warembo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za ushiriki.
“Tunawaalika warembo wote kutoka Kata zote zilizopo chini ya Chang’ombe kujitokeza bila kuogopa ilimradi wawe na vigezo stahiki. Fomu za kujiunga ili kushiriki katika shindano la Miss Chang’ombe zinapatika pale CDS PARK (TCC Club) Chang’ombe, MPOAFRIKA Davis Kona, na duka la nguo CHILU Latest Wear Temeke Mwisho. Karibu sana” alitoa wito Bwana Adam Hussein.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya SG, Bwana. Geofrey Mbalazi aliomba wadau na wadhamini kujitokeza kwa wingi kwani nafasi zipo wazi. Ambapo alieleza kuwa hadi sasa wameoata wadhamini kadhaa wakiwemo kutoka DATASTAR TRAINING COLLEGE, CDS PARK, MPOAFRIKA, NATIONAL HOTEL na CHILU Latest Wear.
Kuhusu SG Entertainment:
Kampuni ya SG Entertainment imesajiliwa na BASATA kupewa kibali kuendesha shughuli za Sanaa nchini Tanzania. Imeshafanya shughuli mbalimbali za sanaa ikiwemo mashindano ya urembo mbalimbali tokea kuanzishwa kwake na ni miongoni mwa makampuni yenye sifa kubwa katika kuendeleza tasnia ya Sanaa haoa nchini ambapo ikiwa inaongozwa na vijana wenye weredi mkubwa wa masoko, Habari na mawasiliano pamoja na Sanaa kwa ujumla ya ndani na nje.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Bwana. Victor Mkumbo (kushoto) akizungumza kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo wa Miss Chang’ombe 2016. Kulia ni Mratibu wa shindano hilo, Bwana Adam Hussein .
Mkutano huo ukiendelea..
Mratibu wa shindano hilo la Miss Chang’ombe, Bwana Adam Hussein (kulia) akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) juu ya shindano hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Bwana. Victor Mkumbo
Baadhi ya warimbwende wakiwa kwenye pozi wakati wa utambulisho huo
Mratibu wa shindano hilo la Miss Chang’ombe, Bwana Adam Hussein (Katikati) akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) juu ya shindano hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Bwana. Victor Mkumbo na Kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya SG, Bwana. Geofrey Mbalazi
Baadhi ya warembo hao wa Miss Chang’ombe wakiwa katika pozi hilo
Mmoja wa warembo hao wa Miss Chang’ombe akiwa katika mahojano wakati wa utambulisho huo wa shindano la Miss Chang’ombe.
Mahojiano yakiendelea..
Baadhi ya warembo hao wa Miss Chang’ombe wakiwa katika pozi wakati wa utambulisho wa Shindano la Miss Chang’ombe. Waandaaji wa shindano hilo wametoa wito kwa wanadada wengine kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kushiriki shindano hilo. Ambapo vigezo ni umri wa kuanzia miaka 18 hadi 24 na awe mkazi wa Kitongoji cha Chang’ombe ama ndani ya Kata zilizo katika Kitongoji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
The post Kampuni ya SG Entertainment yafanya utambulisho wa Miss Chang’ombe 2016 appeared first on DEWJIBLOG.