Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin ataonesha mitindo yake kama mgeni mwalikwa kwenye tukio la mitindo la “Plus Size Fashion Show” inayo tegemea kufanyika Visiwani Zanzibar siku ya Jumamosi ya Oktoba 8 2016 katika Hotel ya Grand Palace.
Asya ni mmoja wa wanamitindo wakubwa nchini Tanzania ambaye amejizolea umaalufu mkubwa kupitia kazi hizo za mitindo hivyo kupitia kampuni ya mitindo ya Zanzibar inayo tambulika kama “Style House” chini ya Mkurugenzi wake Mkuu Mama Titi ambaye anaishi uingereza itakuwa chachu kwa wabunifu wengine kujifunza kutoka kwake pamoja na kupata uzoefu wa kutosha.
Ingawa Asya anaishi Marekani lakini kwa sasa yupo  hapaTanzania kwa  ajili ya onesho hilo lenye dhumuni kubwa la kuchangia “Breast Cancer Zanzibar” Mbali na Mama wa mitindindo, designers wengine pia watashiriki kikamilifu  kwenye ufanisi Onesho hilo.
Special Apperance atakuwa ni mwigizaji Wastara Sajuki, Burudani itatolewa na  Khadja Kopa huku watu mbalimbali wanakaribishwa.


The post Mama wa Mitindo Asya Idarous kupamba jukwaa la “Plus Size Fashion Show” Zanzibar appeared first on DEWJIBLOG.