Quantcast
Channel: Fashion – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Swahili Fashion Week 2016 kufanyika Desemba 2-4 Dar,Wabunifu 40 kupamba

$
0
0

LEO Novemba 9.2016. Katibu Mtendaji wa Basata, Bwana Godfrey Mungereza ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinudizi rasmi wa SWAHILI FASHION WEEK na Tuzo kwa mwaka 2016 amepongeza juhudi za Waandaaji wa maonyesho hayo kwani yamekuwa yakiinua taalum ya Ubunifu hapa nchini na kuongeza fursa za ajira.

Bwana Mungereza amebainisha kuwa, bila maonyesho kama hayo Taifa halitapiga hatua katika tasnia ya utamaduni, Sanaa na Ubunifu hivyo uwepo wake maonyesho hayo unasaidia kuinua sekta hiyo ambayo pia inaongeza ajira kwa wananchi wake.

Katika tukio hilo, Mungereza aiweza kuzindua rasmi nembo ya Swahili Fashion Week kwa 2016 huku na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wengine kama akina Mustapha Hassanali ilikuendeleza fani ya ubunifu hapa nchini.

Naye Mustafa Hassanali ambaye ni mwanzilishi wa maonyesho hayo ameeleza kuwa licha ya kuwa na changamoto mbalimbali tokea kuanzishwa kwake hiyo mwaka 2008, Wameweza kuinua uwezo pamoja na kuibua vipaji kwa wabunifu mbalimbali nchini.

“Si kwamba tu tulionyesha dunia kuwa kina cha vipaji vya ubunifu  nchini Tanzania na Afrika ni vya ajabu kweli. Lakini sasa tuna wadau na watu mbalimbali wakilisubiria kwa hamu kuliona onyesho hili la SWF” ameeleza Mustafa Hassanali.

Kwa upande Meneja Masoko wa maonyesho hayo, Hamisi Omary amesema ni wasaha mzuri  kwa wafanyabiashara za ubunifu na mavazi na vitu mbalimbali kujitokeaza katika kufanya biashara na onyesho hilo ambalo limekuwa likistawi kila mwaka tokea kuanzishwa kwake hapa nchini.

Pia ameongeza kuwa, katika onyesho hilo la siku tatu, nyakati za mchana kutakuwa na tamasha laununuzi wa bidhaa ambapo wafanyabishara na wadau wengine watakuwa wakiuza bidhaa zao na jioni ni maonyesho ya mavazi ya jukwaani.

Pia kutakuwa na utoaji wa tuzo 24 kwa wabunifu shiriki.

SWF 16, kwa mwaka huu ni awamu ya tisa (9) kuendelea kufanyika kwa maonyesho hayo ya ubunifu ambapo wabunifu 40 wanatarajiwa kuonyesha mavazi hayo ya ubunifu.

Huku tukio hilo likitarajia kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta, jirani na Chuo cha IFM, Jijini Dar es Salaam.

SWF 16, imeandaliwa na 360 degrees huku ikidhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Darling Hair, Colosseum hotel &Spa, BASATA na wengine wengi.

Na Andrew Chale,MO BLOG

dsc_0230Mwanzilishi wa Swahili Fashion Week, Mustafa Hassanali akiwatambulisha wageni akiwemo Mgeni rasmi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza anayemfuatia. wengine ni wawakilishi kutoka Colesseum Hoteli, Bi. Tanya Vissel,  akifuatiwa na Deus Kakuru kutoka kampuni ya Darling Hair

dsc_0232Mgeni rasmi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza (kulia) wakiwa katika hatua za ufunguzi rasmi

dsc_0233 dsc_0235 dsc_0243Tayari limefunguliwa rasmi SWF16

dsc_0247Mgeni rasmi kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mungereza akizungumza namna Sanaa ya Ubunifu hapa nchini inavyokuwa kwa kuendelezwa na wabinifu wa ndani

dsc_0248 dsc_0255 dsc_0259Muonekano wa logo, mpya ya Swf 2016

dsc_0260 dsc_0261Meneja Masoko wa maonyesho ya SWAHILI FASHION WEEK, Hamisi Omary akizungumza katika tukio hilo

dsc_0269Tukio hilo likiendelea.

swaf16Baadhi ya wabunifu: Kulwa Mkwandule (wa kwanza kushoto) akifuaatiwa na Mbunifu Martin Kadinda wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa utambulisho wa baadhi ya wabunifu hao watakaoshiriki SWF16

dsc_0298 dsc_0305Baadhi ya wabunifu watakaoshiriki katika SWF16 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mapema leo Novemba 9.2016.

PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE

The post Swahili Fashion Week 2016 kufanyika Desemba 2-4 Dar,Wabunifu 40 kupamba appeared first on DEWJIBLOG.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Trending Articles