Quantcast
Channel: Fashion – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Vodacom kuwaunga mkono wanamitindo nchini

$
0
0

fashion vd

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda,(kushoto)akikabidhi Tuzo ya Programu bora ya fasheni ya mwaka kwa waongoza kipindi cha “NIVARNA”kinachorushwa na EATV.

Zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya kumalizika kwa mafanikio maonesho ya mitindo ya Swahili Fashion week, mdhamini wa maonesho hayo kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeahidi kuendelea kuwaunga mkono wanamitindo nchini na kuwasaidia kufikia malengo yao.

Akizungumzia mafanikio katika maonesho hayo, Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda amesema kampuni yake imekuwa mdau mkubwa katika kuwaunga mkono wanamitindo nchini.

“Ubunifu wa mitindo ya mavazi imekuwa ni ajira kwa mamia ya Watanzania ambayo inawalipa vizuri tu, inavutia kuona tasnia hiyo ikikua kwa kasi ya ajabu huku sisi tukiwa ni sehemu ya ukuaji huo. Siku zote tumekuwa tukiunga mkono shughuli hizi nchini na ninaahidi kuendelea kufanya hivyo kwani kwa pamoja tukishirikiana sisi na wabunifu wetu ndipo tunaweza kuitangaza nchi yetu katika ulimwengu wa wabunifu.” Alisema Kamuhanda

Aliongezea pia “kuna watu wengi wenye vipaji na wanahitaji udhamini wetu ili kupata fursa ya kudhihirisha uwezo wao. Tumejidhatiti kufanya nao kazi bega kwa bega kuhakikisha hilo linafanikiwa, tunawaomba na wao waongeze bidii kuwa wabunifu zaidi kwa kubuni mavazi ambayo si yatawatagaza wao bali na taifa kwa ujumla.” Alisema Kamuhanda na kumalizia kuwa “Tunanataka ifikie hatua nchi yetu inakuwa ni sehemu ya wanamitindo mbalimbali kujifunzia, vilevile nawaomba watanzania waunge mkono kazi za nyumbani, tuachane na kuthamini vya watu tujaribu kuwa wazalendo zaidi.”

moja swahi

Robert Harrison ambaye alikuwepo siku ya maonesho hayo alisifu jinsi tamasha hilo lilivyaoanyika na kupongeza kwa kiasi kikubwa juhudi zilizofanywa na waandaaji kwa kushirikiana na wadhamini wao.

“Nimefurahi sana kuhudhuria tukio hili, nimevutiwa sana na uwezo wa wabunifu wetu wa nyumbani kwa kweli sasa tunaweza kushiriki kimataifa na kushinda. Kwa dunia ya sasa hivi muonekano na mpangilio wa kimavazi una nafasi yake katika maisha yetu. Ninapenda kuvaa na kuonekana nadhifu lakini siwezi kufanikiwa hilo bila ya kujua wabunifu wetu wanatengeza mavazi gani, wanashauri nini kikivaliwa na nini ndio mtu hupendeza, hawa si wabunifu tu bali ni washauri juu ya namna ya mavazi.” Alimalizia Robert

Onesho hilo kubwa lilifanyika kwa siku tatu mfululizo liliteka jiji la Dar es Salaam huku ikishuhudiwa wanamitindo mbali mbali ndani na nje ya nchi wakionesha mavazi ya jukwaani lilivuta hisia za mashabiki wengi wa tasnia hiyo nchini.

ttau swahili


Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Trending Articles