Quantcast
Channel: Fashion – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

TaSUBa yatangazia umma nafasi za kozi kwa mwaka wa masomo 2015 /2016

$
0
0

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

(TaSUBa)

timthumb

TANGAZO LA KUJIUNGA NA CHUO

TaSUBa inawatangazia umma nafasi za kujiunga na kozi kwa ngazi ya Cheti (Certificate) na

Stashahada (Diploma) kwa mwaka wa masomo 2015 /2016

 Kozi hizo ni kama ifuatavyo:-

  1. Sanaa za Maonyesho (Performing Arts):-

Muziki, Ngoma, Tamthiliya/Maigizo, Sarakasi na Sanaa za Ufundi

  1. Ubunifu na Uzalishaji wa Muziki (Music Design and Production)
  2. Picha Jongefu (Media Design and Film Production)

    – Masomo ya sayansi ya Jamii, ICT, Kiswahili na Kiingereza yatafundishwa kwa wote.

   – Mwombaji kozi namba mbili (2) na namba tatu (3) awe na ujuzi wa compyuta.

unnamed (3)Pichani miongoni mwa walimu wa TaSUBa wakionyesha igozo la ubunifu jukwaani chuoni hapo.

NGAZI  YA CHETI KWA MIAKA MIWILI

Sifa za Kujiunga

-    Aliyemaliza Darasa la Saba (Standard Seven) na ambaye hakuhitimu kidato cha Nne

-    Aliyehitimu kidato cha Nne na hakufanikiwa kupata wastani wa “D” nne (4)

ANGALIZO:

-     Ngazi hii ni kwa Masomo ya Sanaa za Maonyesho TU.

-     Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM B

IMG_0404.jpg wanafunziBaadhi ya wanafunzi wa TaSUBa wakiwa katika moja ya shughuli za ngoma katika jukwaa chuoni hapo.

 NGAZI YA CHETI KWA MWAKA MMOJA

Sifa za Kujiunga

-    Aliyemaliza kidato cha nne na kupata wastani wa “D” nne (4)

ANGALIZO:

-    Watakaofaulu wastani wa ‘B’ baada ya kuhitimu ngazi ya cheti wataruhusiwa kujiunga

na Stashahada (Diploma) kwa miaka miwili.

-    Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A

 a78f38f1d4L

Wanafunzi wa TaSUBa wakiwa darasani chuoni hapo.

NGAZI YA STASHAHADA (DIPLOMA)

Sifa za Kujiunga

-    Awe amefaulu kidato cha sita na kupata principal pass 1 na subsidiary 1

-     Awe  amehitimu  ngazi  ya  cheti  cha  sanaa  za  maonyesho  na  ufundi  kwenye  chuo kinachotambuliwa na NACTE

ANGALIZO:

-    Waombaji wa Ngazi hii watajaza FORM A

IMG-20130928-WA0000Miongoni mwa wasanii Mahiri hapa Nchini Tanzania, Baba Haji akiwa katika pozi wakati wa kuhitimu masomo yake. Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii waliopitia chuo hicho. 

MAELEZO MENGINE

-    FOMU za kujiunga zinapatikana Chuoni pia kwenye tovuti ya chuo www.tasuba.ac.tz

-     Kila mwombaji atalipia ada ya FOMU ya Tsh.15,000/=kupitia NMB BANK akaunti

       Na. 2101100012 yenye jina UTAWALA CHUO CHA SANAA

-    Maombi yaambatanishwe na stakabadhi ya malipo (Receipt/Bank Pay Slip) ya Tsh.

15,000 kwa ajili ya FOMU.

-     Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31/05/2015 na maombi yote yatumwe kwa; MTENDAJI MKUU, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania.

-    Kwa MAELEZO zaidi wasiliana nasi kupitia namba za simu: 0715974100, 0763408792,  na 0715394933 au Barua pepe  taasisisanaa@gmail.com


Viewing all articles
Browse latest Browse all 244