Miss Universe wa Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach katika picha ya pamoja washiriki wenzake wa Miss Universe 2015 baada ya kuvikwa taji hilo.(Picha kwa hisani ya @MissUniverse).
Miss Universe wa Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach.
Miss Universe wa Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach katika ubora wake.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss Universe wa Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach ameshinda taji la Miss Universe 2015 katika fainali ya mashindano hayo yamefanyika usiku wa jumapili, Planet Hollywood Las Vegas Resort & Casino nchini Marekani.
Pia amewashinda wenzake Miss Universe wa Colombia, Ariadna Gutierrez aliyekamata nafasi ya pili na Miss Universe wa Marekani, Olivia Jordon aliyeshikilia nafasi ya tatu ya mashindano hayo.
Pia aliwashinda wenzake baada ya majaji kuwauliza “Kwanini unataka kuwa Miss Universe 2015?” na Pia kujibu “Kuwa Miss Universe ni kuwa na mambo mawili, moja heshima na nyingine uwajibikaji, nitatumia sauti yangu kuwashawishi vijana na kuwapa uelewa kuhusu HIV kwa muda wangu na mambo mengine nikiisaidia nchi yangu Ufilipino, nataka kuinyosha dunia kuwa Miss Universe ninajiamini na ninauzuri kuanzia moyoni”
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi Pia alivishwa taji na Miss Universe 2014, Paulina Vega wa Colombia.
Awali mwendeshaji wa sherehe hiyo Steve Harvey alikosea kumtangaza mshindi na kumtaja Miss Universe wa Colombia, Ariadna Gutierrez lakini aliomba msamaha kwa kufanya makosa hayo na kurekebisha.
Tanzania katika mashindano hayo iliwakilishwa na Lorraine Marriott ambaye hakufanikiwa kuwika kwenye fainali hiyo.