Quantcast
Channel: Fashion – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Wema Sepetu awafunda wabunifu chipukizi wa Lady In Red fashion show 2016

$
0
0

DSC_0805

Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya Idarous Khamsin (katikati) akimtambulisha rasmi mwanadada, Wema Sepetu (kushoto) ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. (Kulia) ni Martin Kadinda ambaye naye miongoni mwa watendaji wanaoratibu jukwaa hilo la Lady in Red. katika usiku wa Lady In Red fashion show 2016, litakalofanyika 31 Januari ndani ya ukumbi wa Danken House wa Mikocheni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog

Nyota wa filamu za Bongo, ambaye pia aliwai kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Wema Issac Sepetu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye onesho na jukwaa maalum la mitindo la kila mwaka la “Lady In Red 2016”  litakalofanyika 31 Januari katika ukumbi wa Danken House uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Fabak Fashions na mwandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asya Idarous Khamsin amebainisha hilo alipokutana na badhi ya wabunifu wa mavazi na wanamitindo watakaopamba jukwaa hilo hiyo 31 Januari, ambapo amewataka kujipanga ilikuchangamkia fursa ya kupata kuinua tasnia ya mitindo nchini.

“Lady In Red fashion show 2016 ni ya kipekee na jukwaa hili ni fursa kwa kuinua wabunifu wa mavazi chipukizi kupata kuonekana zaidi na hata kukuza majina na ubunifu wao kujulikana ndani na nje” amefafanua Mama wa Mitindo, Asya Idarous.

Aidha, ameeleza kuwa, ilikutoa msisimko zaidi kwa jukwaa hilo. Mwanadada Wema Sepetu ndiye atakaye bariki siku hiyo ikiwemo utoaji wa vyeti kwa washiriki ilikuweka kumbukumbu.

Asya Idarous ameongeza kuwa, hadi sasa jukwaa hilo la Lady in red linafikia umri wa miaka 12 litaendelea kuwa juu zaidi na kuwa shule kwa tasnia ya mitindo ambapo kwa sasa pia linafanyika na nje ya Tanzania ikiwemo nchini Uingereza.

Hata hivyo  wadau mbalimbali  wameombwa kujitokeza kuliunga mkono ikiwemo kudhamini onesho hilo.


DSC_0810

Mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady Inn Red fashion show 2016 kama inavyoonekana pichani.

DSC_0808

Mwanadada Wema Sepetu akitoa nasaha zake kwa Wabunifu wa mavazi na wanamitindo (hawapo pichani) wakati wa utamburisho wa jukwaa la Lady In Red fashion show 2016 linalotarajiwa kufanyika 31 Januari.

DSC_0793

Martin Kadinda akitoa nasaha zake kwa wabunifu na wanamitindo waliojitokeza katika mkutano huo (hawapo pichani) kuhusiana na jukwaa la Lady In Red fashion show 2016.

DSC_0865

DSC_0903

Wabunifu wa mavazi na wanamitindo wakifuatilia mkutano huo wa utambulisho wa jukwaa la Lady In Red fashion show 2016.

DSC_0760

Baadhi ya wabunifu wa mavazi na mitindo wakifuatilia mkutano huo.

DSC_0881

DSC_0898

DSC_0873

DSC_0888

DSC_0885

DSC_0904

DSC_0765

DSC_0760

DSC_0902

DSC_0816

..Wakipata ‘selfie’ na Wema Sepetu

DSC_0833

..Wakipata ‘selfie’ na Martin Kadinda

DSC_0921

DSC_0830

Picha ya pamoja…


Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Latest Images

Trending Articles



Latest Images