Tasnia ya mitindo na ubunifu nchini Tanzania imeendelea kukua siku baada ya siku huku wabunifu wa fani hiyo wakiongezeka mara dufu. Mwishoni mwa wiki iliyopita ilifanyika tukio moja kubwa nalo ni la kutunuku vyeti wabunifu na washiriki waliofanikisha majukwaa ya Lady In Red fashion show 2016 yaliyofanyika Dar es Salaam Januari 31 na lile lililofanyika London, Uingereza, Februari 13.
Katika tukio maalum la kuwapongeza na kuwatunuku vyeti lililojulikana Lady In Red 2016 After Party iliyofanyika ndani ya Regency Park Hotel, wabunifu hao chipukizi walimshukuru Mama wa Mitindo Asya Idarous kwa kuweza kuwainua kupitia tasnia hiyo huku wakimwelezea kuwa ni Mama wa mfano.
Wabunifu hao wamemwelezea kuwa, awali walijiona wachanga zaidi na hata kutojiamini lakini kwa kupitia majukwaa ya Lady In Red yameweza kuwatia moyo na hata kuweka malengo yao ya kufikia kule wanakotaka katika majukwaa ya ubunifu na mitindo hapa nchini.
Pichani ni baadhi ya picha wabunifu hao wakikabidhiwa vyeti vyao..
Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani Mbunifu wa mavazi na mitindo, Salim.
Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamsin akimkabidhi cheti cha shukrani Mbunifu wa mavazi na mitindo, Jastin. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).
The post Wabunifu chipukizi (Designers) wamshukuru Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamsin appeared first on DEWJIBLOG.