Quantcast
Channel: Fashion – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Mtazania ashinda taji la mrembo wa gereza

$
0
0

Mashindano maarufu ya Mrembo wa Gereza katika Gereza la Lang’ata yamelenga kuwasaidia wafungwa wakike kupata afueni ya kisaikolojia na kurudi katika hali zao za zamani kabla ya kifungo.

Shindano hilo la urembo limelipa gereza la Lang’ata umaarufu mkubwa baada ya video za mashindano hayo kurushwa katika mitandao ya kijamii mbalimbali duniani.

Katika mashindano hayo ya mrembo wa gereza Mtanzania Tina Martin ameshika nafasi ya pili ya taji la mrembo wa Gereza akipitwa kwa spidi ya mwendo kasi na mwanadada wa Kikenya Ruth Kamande.

Mtanzania  huyo amehukumiwa kifungo katika Gereza hilo baadaya kukutwa na tuhuma za kuingiza madawa ya Kulevya kwa njia za magendo nchini Kenya.

Ruth Kamande amewapiku washindani wenzake 19 na kutwaa taji la mrembo wa Gereza la Lang’ata , mashindano ambayo yanafanyika kila mwaka gerezani hapo.

Ruth Kamande ni binti wa Kikenya mwenye umri wa miaka 21 ambaye alihukumiwa kwenda jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake bwana Farid Mohammed.

Bi Ruth alifanya tukio hilo nyumbani alipoishi na mpenzi wake eneo la Buruburu Jijini Nairobi mnamo mwaka 2015, baada ya kuona kile kinachodaiwa kuwa ni ujumbe wa kimapenzi kwenye simu ya mpenzi wake  kutoka kwa mwanamke mwingine (Mchepuko).Bw Farid alipoteza maisha akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta –KNH.

Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).

Tazama hapa kushuhudia tukio hilo:

4_66Baadhi ya warimbwende hao wakiwa katika furaha wakati wa kutengenezwa nywele zao kabla ya kuelekea kwenye shindano hilo

5_44Baadhi ya washiriki wa shindano hilo wakiwa jukwaani wakati wa shindano hilo la mrebo wa gereza

mashManjonjo ya urembo jukwaani yakiendelea

mashindano mashfrrrMrembo wa Gereza la Lang’ata, Ruth Kamande ambaye amewapiku washindani wenzake 19 na kutwaa taji hilo la urembo akiwa amekaa na taji lake hilo la ushindi huku washindi wa pili Mtanzania (kulia) Tina Martin na kushoto mshindi wa tatu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa.

tina-martib

Mrembo wa Tanzania kwenye gereza hilo, Tina Martin akiwa kwenye pozi

rutjjh-2Mrembo wa Gereza la Lang’ata, Ruth Kamande  akiwa kwenye pozi na baadhi ya askari wa Magereza wa Kenya wakati wa ushindi wake huo wa kutwaa taji hilo la urembo  wa gereza. 

3_81Mrembo wa Gereza la Lang’ata, Ruth Kamande ambaye amewapiku washindani wenzake 19 na kutwaa taji hilo la urembo akiwa kwenye pozi. 

 

The post Mtazania ashinda taji la mrembo wa gereza appeared first on DEWJIBLOG.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Trending Articles