Quantcast
Channel: Fashion – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Wabunifu mbalimbali kupamba miaka 10 ya ‘Lady in red’ Februari 14

$
0
0

asia leo

-Magwiji, chipukizi watajwa

-Magwiji wamo ..Ally Remtullah, Khadija Mwanamboka, Mustapha Hasanali, Martin Kadinda

-Chipukizi wamo…Faustin Simon,Waiz Shelukindo, Agusta Masaki

Na Andrew Chale

WABUNIFU mbali mbali watakaopamba miaka 10 ya onyesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Lady in Red Super brand, 10th Anniversary’ linalotarajiwa kufanyika Februari 14, tayari majina ya wabunifu hao yamewekwa hadharani.

Jukwaa hilo la Lady in red, ndiyo linaongoza kwa kuibua vipaji vya wabunifu maarufu hapa nchini tokea kuanzishwa kwake miaka 10 iliyopita huku wabunifu hao wakongwe na chipukizi, wakipata kuonekana na kuonyesha uwezo wao.

Onyesho la mwaka huu linatarajia kufanyika kweney hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam, Februari 14, huku vazi maalum likiwa ni jekundu kwenda na siku hiyo ya wapendanao.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions inayoandaa onyesho hilo , Asia Idarous Khamsin, alisema kila mwaka onyesho hilo huja kitofauti ikiwemo kuongeza vionjo mbalimbali katika kufikia mafanikio kweney tasnia ya ubunifu na mavazi hapa nchini.

“Safari hii, steji ya Lady in red’, inatimiza miaka 10, huku ikijivunia kuibua vipaji vya wabunifu wengi hapa nchini, ambao kwa sasa wanamajina makubwa kwenye kazi zao, hivyo tutaendelea kutoa nafasi kwa wabunifu wetu hapa nchini ilikukuza tasnia hii” alisema Asia Idarous.

Asia Idarous aliwataja wabunifu magwiji watakaopamba steji hiyo kuwa ni pamoja na Khadija Mwanamboka, Mustapher Hasanal , Ally Remtulla, Lucky Creation, Martin Kadinda, Ghymkana Paka wear, Gabriel Molel, Fransiska Shirima, Salim Alii, Amid Abdul, Kikis Collection, Rose fashion, Diana Magesa, Rio Paul na wengine.

Kwa upande wa wabunifu chipukizi watakaopamba ni pamoja na Faustin Simon, Water Edward, Brian Hango, Benedict Mnzava,Crissiwelly Willex, Silliness Jackson, Gumbala, Jabir Jumanne, Alabama King, Agusta Masaki, Nelson Tomas, Beni Juliet,Ummi fashion, Asmahan Eva, Hassan Nasor, Juniper Mafuru, Ante Ngongi, Adam Hassan Kijangwa na Waiz Shelukindo.

Aidha, Asia Idarous aliongeza kuwa, kwenye onyesho hilo, pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo kutoka bendi ya Babloom Trio na Mwanamuziki mahiri wa nyimbo na ngoma za asili, Wanne Star. Katika onyesho hilo ambalo litafanyika siku hiyo ya Februari 14, ambayo pia itakuwa ni siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’ , kiingilio kitakuwa sh 30,000 kwa viti vya kawaida huku viti maalum ikiwa sh 50,000.

Tayari tiketi za onyesho hilo zimeanza kuuzwa ikiwemo vituo vya duka la Fabak fashion, lililopo mikocheni mkabala na kituo cha Mwalimu Nyerere huku kwenye hoteli ya Serena, zikipatikana mapokezi.

Kwa upande wa wadhamini wakuu wa shindano hilo ni pamoja na kinywaji cha Zanzi pamoja na kampuni ya nywele ya Darling. Wengine ni CXC, Times fm, Clouds media, Vijimambo blog, michuzi media group, channel ten, Elite Computer, Eventlites, One touch-solution, Raysa Style, Paka Wear, Dj Bula, Magic fm, DTV, Jambo Leo, I View media, Vayle Spring, Voice of American na wengine wengi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 244

Trending Articles