Jana Juni 5.2016, kulifanyika kilele cha maonyesho na Mavazi ya stara, Stara fashion Week 2016 ndani ya ukumbi wa City Garden Restaurant uliopo Kamata.
Mbali na mitindo ya Stara, pia bidhaa mbalimbali ziliuzwa kwa mahitaji ya wanawake wanaume na watoto kwa manunuzi ya vitu mbalimbali, kama vile Mabaibui,Mitandio Madera kwa ajila ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani, evening dresses, kanzu, Udi Vyetezo na vitu vingine pia kulikuwa na wchora heena kwa bei nafuu.
Ungana na Andrew Chale katika picha bora za awali kwenye tukio hilo hapa:
Mbunifu wa mavazi anayefanya vizuri, Mkwandule akinadi mavazi yake katika jukwaa hilo la Stara fashion Week 2016
Imam Qasim kutoka Houston Texas, Marekani alikuwa mgeni rasmi ambapo pia alizindua chapisho la toleo la kitabu cha Stara 2016.
Imam Qasim alitoa wito kwa Waislam wote kufanya mambo mema kwa kipindi chote ikiwemo kwa mwanamke kujistiri hasa mavazi ya Stara kama ilivyo kwenye vitabu takatifu.
Mbunifu wa mavazi, Mwandule akichukua vipimo vya moja ya mishono kwa mteja ambaye alipenda kazi zake katika jukwaa hilo ambapo wateja mbalimbali walinunua kazi za wabunifu waliokuwa wakishiriki jukwaa hilo.
Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog.
Picha zaidi zinakuja
The post EXCLUSIVE: Picha za jukwaa la Stara Fashion Week 2016 zipo hapa appeared first on DEWJIBLOG.