WIKI ya maonyesho na Mavazi ya stara, Stara fashion Week 2016 ita kuchukua nafasi yake tena mwaka huu katika ukumbi wa City Garden Restaurant uliopo Kamata, ambapo tukio zima lilianza kuanzia June 1 na leo Juni 5 ni kilele cha jukwaa hili.
Awali litafunguliwa na Exhibition ya bure, linakaribisha watu mbalimbali wanawake wanaume na watoto kwa manunuzi ya vitu mbalimbali, kama vile Mabaibui,Mitandio Madera kwa ajila ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani, evening dresses, kanzu, Udi Vyetezo na vitu vingine pia kutakuwa na wachora heena kwa bei nafuu.
Katika tukio la leo maonyesho ya mavazi ya stara kwa wanawake pekee ambapo tukio la aina yake litaanzia saa nne hadi saa 11 jioni.
Katika kilele cha maonyesho haya kazi za mikono ya wabunifu wa hapa nyumbani wanaobuni mavazi ya stara zitaonyeshwa pamoja na warsha itakayojadili mada mbalimbali ambazo ni pamoja na
1. Jinsi ya kumpata mwenza na kudumisha ndoa
2. Matumizi na Mipango ya Fedha
3. Ujasiriamali Na nyinginezo
Kongamano hili la wanawake, litakuwa na kiingilio cha shilling elfu 35 VIP na Elfu 50 viti maalum Kwa kujumuisha chakula cha mchana kwa wote na zawadi mbalimbali zitatolewa.
Stara fashion week imedhaminiwa na TSN group, Maximalipo, Hijab Couture, Hijabi Central Tz, Kanzu Point, Cordoba School, Speedy Print, I-view Studio, Vayle Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden Restaurant, Event Lights, Sofia Production, Clouds Media na wengineo.
Moja ya mavazi ya Stara katika matukio ya jukwaa hilo
The post Jukwaa la mitindo la kila mwaka la Stara Fashion Week kufikia kilele leo Juni 5 appeared first on DEWJIBLOG.