Baada ya mama wa mitindo Asya Idarous Khamsin kuendelea kufanya vizuri huko Marekani kwa kufanya Fashion Show kadha wa kadhaa ikiwemo ile ya “Dicota 2016” Habari njema mwanamitindo huyu amerejea nchini Tanzani siku chache zilizo pita kwa ajili ya Fashion Show kubwa maarufu kama “Stara Fashion Week” inayotegemea kufanyika hapo kesho siku ya Jumapili 5/6/2016 ndania ya “City Garden Restaurant”.
Kumbuka vazi hilo litaoneshwa na kuuzwa siku hiyo hiyo kwa watakao hitaji, kiingilio ni 30,000 kwa watu wa kawaida 50,000 kwa VIP muda ni kuanzia saa 10 asubuhi mpaka 11 Jioni Lunch itatolewa bureeee! nyote mnakaribishwa.
Tiketi za jukwaa hilo la Stara fashion week
Moja ya kazi za Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamisin
Baadhi ya mavazi ya Stara yatakayokuwapo kwenye jukwaa hilo na mengineo mengi kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asya Idarous Khamisin
The post Mama wa mitindo Asya Idarous Khamisin kushiriki jukwaa la Stara fashion Week 2016 appeared first on DEWJIBLOG.